1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vini Jr. aisaidia Real kuipiga Atletico

19 Septemba 2022

Kulishudiwa baadhi ya mashabiki wa Atletico Madrid waliorekodiwa kwenye video wakimtolea maneno ya kibaguzi mshambuliaji wa Real Madrid Vinicius Jr. kabla ya mechi dhidi ya Atletico Madrid katika dimba la Metropolitano

https://p.dw.com/p/4H3yn
UEFA Champions League Real Madrid v Manchester City
Picha: Juan Medina/REUTERS

Nchini Uhispania, kuna debi nyingine iliyosubiriwa ya majogoo wa mji wa Madrid. Na hata kukashuhudiwa baadhi ya mashabiki wa Atletico Madrid waliorekodiwa kwenye video wakimtolea maneno ya kibaguzi mshambuliaji wa Real Madrid Vinicius Jr. Nje ya uwanja wao wa Wanda Metropolitano kabla ya kivumbi kutimuliwa jana usiku.

Mamia ya mashabiki wa Atletico walisisika wakiimba Vinicius wewe ni tumbili. Hayo hata hivyo hayakumzuia staa huyo wa Kibrazil kuwasha moto dimbani na kuisaidia Real kupata ushindi wa 2-1. Na Vinicius na mfunga bao Rodrygo walishangilia bao la ufunguzi kucheza densi mbele ya mashabiki wa Atletico.

Kocha Carlo Ancelotti alizungumzia sehemu ya kwanza ya msimu wa La Liga

Mambo mazuri ni kuwa wachezaji wetu wana ushindani mkubwa, na hata bila ya Karim Benzema, ambaye labda ndiye mchezaji muhimu zaidi kwenye timu yetu. Kwa hivyo nadhani hiyo ni nzuri sana. Halafu, kwa upande hasi, kuna mambo ya kuboresha, siku zote kuna mambo ya kuboresha. Lakini ukweli ni kwamba, timu hii inapambana sana, tumeshinda kila mchezo, ni nini kingine ninachoweza kuwaomba wachezaji hawa wafanye? Nina furaha sana, na ninajivunia kuwafundisha wachezaji hawa."

Real wameshinda mechi zao zote 9 katika mashindano yote tangu kuanza msimu huu

afp, ap