1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vinara wa Seria A wapokea kichapo cha 4-0 mbele ya AC Milan

3 Aprili 2023

Kocha wa Napoli Luciano Spalletti amekataa kulaumu kipigo cha 4-0 mbele ya AC Milan kwa kukosekana kwa mfungaji wao bora Victor Osimhen.

https://p.dw.com/p/4PeKx
Fussball I Krzysztof Piatek
Picha: Francesco Scaccianoce/LPS/ZUMA/picture alliance

Klabu ya Napoli inaelekea kutwaa taji lao la kwanza la Seria A tangu enzi za Diego Maradona mnamo mwaka 1990, lakini kikosi cha Luciano Spalletti kilipokea kichapo cha 4-0 dhidi ya AC Milan jana Jumapili.

Mshambuliaji wa AC Milan Rafael Leao alifungua ukurusa wa mabao kabla ya Brahim Diaz na Alexis Saelemaekers kupachika mabao mengine.

Mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 24 ambaye ameifungia Napoli mabao 21 msimu huu, alikosa mchezo huo kutokana na jeraha la paja.

Hata hivyo, licha ya kipigo hicho katika uwanja wao wa nyumbani wa Diego Armando Maradona, Napoli bado imefungua mwanya wa alama 16 kati yao na Lazio inayoshikilia nafasi ya pili na alama 55 wakati AC Milan imetulia katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 51 nayo Inter Milan inafunga ukurusa wa nne bora ikiwa na alama 50.

Vijana wa Spalletti watasafiri hadi Lecce katika mechi nyengine ya Ligi ya Seria A mnamo Aprili 7.

Napoli itapata nafasi ya kulipiza kisasi kipigo hicho wakati itakapotukana tena na AC Milan Aprili 12 katika mechi ya mkondo wa kwanza ya robo fainali ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.