1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VILA YA UGANDA NI MABINGWA WAPYA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

9 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CHZ9

Natuanze na ligi mashuhuri za Ulaya:

Ingawa Bayern Munich imeshatawazwa mabingwa wa Ujerumani tangu wiki iliopita,mshambulizi wao kutoka Holland Roy Makaay yungali ana kiu kikubwa cha kutia magoli:Kwani jumamosi alitia mabao mengine 3 katika ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Mainz.Mwishoni mwa wiki iliotangulia, Makaay alitia pia mabao 3-na kufanya mabao 6 mfululizo katika mashindano 2 yaliopita.

Katika msimu wake wa kwanza katika Bundesliga, Makaay alitia mabao 23,lakini mbrazil Ailton alimpiku kwa mabao 28 wakati akiichezea Werder Bremen-mabingwa waliovuliwa taji msimu huu na Bayern Munich.Makaay ametia sasa msimu huu mabao 19 akiwa nafasi ya pili nyuma ya Mintal wa Nüremberg.Jumamosi ijayo kwahivyo,Mintal atakumbana lango kwa lango na makaay pale timu zao 2 zitakapokumbana kukamilisha msimu huu wa Bundesliga.

Mabingwa wa msimu huu-Werder Bremen wamepoteza matumaini yote ya kuambulia alao nafasi katika Champions League-msimu ujao.Jana walichapwa bao 1:0 na Borussia Dortmund.

Ni msimu uliopita tu ambapo bremen ilitwaa vikombe vyote 2 vya Ujerumani-ligi na Kombe la shirikisho la dimba.

Katika Premier League-Ligi ya Uingereza, Chelsea ilikabidhiwa jana Kombe lao kufuatia ushimndi wao wa bao 1:0 dhidi ya Charlton Athletic.Bao lao la dakika ya mwisho ya 90 lilitiwa na Claude Makelele.

Arsenal,imetiwa shime kwa ushindi wao wa mabao 3:1 dhidi ya Liverpool na wana matumaini sasa ya kuibuka makamo-bingwa wa Uingereza nyuma ya Chelsea.

Olympique Lyon wametawazwa nao mabingwa wa Ufaransa kwa mara ya 4 mfululizo-hii inafuatia ushindi wao wa mabao 2:1 nyumbani dhidi ya AJ Ajaccio zikibakia mechi 3 tu kumaliza msimu.

Hata Fc Barcelona ya Spain imepiga hatua karibu kutwaa ubingwa wa Spain ilipoizaba jana valencia mabao 2:0.Mkamerun Samuel Eto’o anaendelea kuongoza orodha ya watiaji magoli kwa mabao yake 23.Ronaldo anafuata nafasi ya pili kwa mabao 20.

Ama Ligi mashuhuri za Afrika,zilimalizika mwishoni mwa wiki hii kwa:

Kaiser chief na Orlando Pirates zikiwa zikishindana kunyan’ganyia taji la Afrika Kusini.Timu zote mbili zilitamba mwishoni mwa juma :Hatahivyo, Orlando iko pointi 6 mbele ya Kaiser Chiefs.Pirates iliikomea jana Wits University bao 1:0 wakati siku moja kabla hapo jumamosi,Kaiser chiefs iliizaba Moroka Swallows mabao 2:0 mjini Johannesberg.

Huko Nigeria:Enyimba-mabingwa wa Africa waliitandika Iwuanyanwu Nazionale mabao 3:0 na sasa wanaongoza Ligi ya Nigeria kwa pointi 4.

Katika ligi ya Ghana, Feynoord Acadamy ilizimwa jana sare 0:0 na Asante kotoko.Hatahivyo, Feynoord iko kilerleni mwa Ligi.Nchini Angola, SARGADA ESPERENCE imeshika usukani wa Ligi baada kuizaba Benefica Luanda jana 2:0.ASEC Abidjan iliitandika Stella Abidjan bao 1:0 katika kiu chao cha kuvaa taji kwa mara ya 6 mfululizo.

KOMBE LA KLABU BINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI:

Kinyan’ganyiro cha kuani taji la kanda hiyo kilimalizika jumamosi kwa Villa ya Uganda kuitimua APR ya Rwanda mabao 3:0.Matokeo hayo kwa kweli yaliwasangaza mashabiki kwavile APR ilianza mashindano haya kwa nguvu,lakini ilibainika baadae kuwa vishindo vyao vya darini viliishia sakafuni.