1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Vikwazo vyainyemelea Niger

30 Julai 2023

Viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi wanakutana hii leo katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, kwa ajili ya mkutano usio wa kawaida wa kilele kuhusiana na mapinduzi ya hivi karibuni ya huko nchini Niger.

https://p.dw.com/p/4UYTr
Nigeria | Bola Tinubu
Picha: Sunday Aghaeze/Nigeria State House via AP/picture alliance

Kwenye mkutano huo wa kilele huenda viongozi hao wakaukabiliana kuiwekea vikwazo Niger.

Kabla ya mkutano huu wa leo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken alizungumza na rais wa Nigeria Bola Tinubu akielezea wasiwasi wake juu ya hali nchini Niger na kusisitiza kuendelea kuunga mkono juhudi za kiongozi huyo za kurejesha utawala wa kikatiba.

Rais aliyechaguliwa wa Niger Mohamed Bazoum amekuwa akizuiwa na jeshi kwa siku nne, na tayari Jenerali Abdourahamane Tiani, aliyekuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais amejitangaza kuwa kiongozi wa taifa hilo.

Tinubu ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo kwa mataifa ya Afrika ya Magharibi, ECOWAS amesema jumuiya hiyo na ya kimataifa wanafanya kila linalowezekana kuilinda demokrasia ya Niger.