1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIKWAZO VIENDELEE LIBERIA

24 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFpq
MONROVIA: Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia Jacques Klein amesema vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Liberia vinapaswa kubakia.Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa akaongezea kuwa ingawa vita vya wenyewe kwa wenyewe vimesita,serikali ya Liberia na uchumi wa nchi hiyo ungali katika hali ya vurugu.Kabla ya kuviondosha vikwazo,Umoja wa Mataifa lazima uhakikishe kuwa utajiri wa taifa unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wake.