1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya usalama vyakabiliana na waandamanaji Chad

19 Mei 2021

Maafisa wa usalama wa Chad wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji katika Mji Mkuu wa nchi hiyo N'djamena waliokuwa wanapinga jeshi kuchukua uongozi kufuatia kifo cha Rais Idriss Deby

https://p.dw.com/p/3td97
Tschad N'Djamena | Proteste und Gewalt
Picha: Sunday Alamba/AP/picture alliance

Ripota mmoja wa shirika la habari la Reuters amesema makundi madogo madogo ya waandamanaji yamechoma magurudumu na bendera za Ufaransa na baadhi wamekabiliana na maafisa wa polisi.

Muungano wa mashirika ya kiraia wa Wakit Tamma umesema watu 30 wamekamatwa.

Msemaji wa polisi Amane Issac Azina amethibitisha kwamba kulikuwa na uharibifu wa mali za umma na kamatakamata ila hakutoa idadi ya waliotiwa nguvuni.