1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Vikosi vya usalama vya Pakistan vyawauwa wapiganaji sita

1 Julai 2023

Jeshi la Pakistan limesema, vikosi vyake vimeyavamia maeneo mawili ambayo ni maficho ya wanamgambo katika mikoa inayopakana na Afghanistan.

https://p.dw.com/p/4TIjK
Afghanistan Chost Gulan Flüchtlingslager Pakistanische Flüchtlinge
Picha: DW/F. Zahir

Tukio hilo lililojiri wakati wa sikukuu ya Iddi, lilipelekea kutokea kwa majibizano ya risasi yaliyosababisha vifo vya wanamgambo sita. Taarifa ya jeshi imeeleza kwamba, operesheni hiyo ilifanywa kwenye wilaya za Tank na Waziristan Kaskazini baada ya kupokelewa kwa taarifa za kuaminika za kijasusi kuhusu kuvamiwa na kufichwa kwa wanamgambo katika maeneo yaliyo karibu na mpaka wa Afghanistan. Wanajeshi wa Pakistan walifanikiwa kukamata silaha na mabomu yaliyokuwa kwenye maficho hayo.

Hata hivyo jeshi halikutoa taarifa zaidi kuhusu utambulisho wa wanamgambo waliouwawa ingawa mara nyingi wapiganaji katika eneo hilo wanatoka katika kundi la Tehreek-e-Taliban Pakistan (TPP), linalofahamika kama Taliban tawi la Pakistani.

Kundi hilo lina mafungamano na lile la Taliban la Afghanistan Tambalo liliingia madarakani katika nchi hiyo jirani Agosti 2021 wakati majeshi ya Marekani na ya Jumuiya ya kujihami ya NATO yalipokuwa kwenye hatua za mwisho za kuondoka nchini humo.