1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMorocco

Uhispania na Uingereza wasaidia shughuli za uokozi, Morocco

11 Septemba 2023

Waokoaji nchini Morocco bado wanapambana kuwatafuta manusura wa tetemeko kubwa la ardhi la usiku wa kuamkia Jumamosi ambalo hadi sasa limesababisha vifo vya watu 2,100 na kufanya uharibifu usiomithilika.

https://p.dw.com/p/4WBlL
tetemeko hilo la nchini Morocco ni kubwa zaidi kushuhudiwa nchini humo.
Manusura wa tetemeko kubwa kabisa la ardhi nchini Morocco lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 akiwa amekaa akilia kwenye kifusi mbele ya nyumba yake iliyoharibiwaPicha: PHILIPPE LOPEZ/AFP

Vikosi vya uokoaji kutoka Uhispania na Uingereza vimejiunga kusaidia juhudi za kuwafikia watu ambao bado huenda wamekwama chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka kutokana na tetemeko hilo lenye ukubwa wa 6.8 katika kipimo cha Richter.

Wengi ya walionusurika na kishindo cha tetemeko hilo lililotikisa wilaya jirani na safu za milima ya Atlas wameendelea kulala nje kwa usiku wa tatu mfufulizo baada ya majengo yao kuporomoka au kuorodheshwa kuwa siyo salama.

Tetemeko hilo linalotajwa kuwa ndiyo kubwa zaidi katika kipindi cha karibu miongo sita limewajeruhi zaidi ya watu 2,000 na kuharibu pia turathi za kitamaduni za Morocco.