1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Umoja wa Ulaya vyafanya mazoezi Uhispania

Josephat Charo
17 Oktoba 2023

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borell, amesema luteka kubwa za kijeshi za Umoja huo zinaendelea kusini mwa Uhispania.

https://p.dw.com/p/4Xe86
Albanien Der Hohe Vertreter der EU für Außen- und Sicherheitspolitik, Josep Borell, auf der gemeinsamen Pressekonferenz in Tirana
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borell.Picha: Press Office, Albania Premiership

Borell amesema wanahitaji kuchukuwa hatua kama inavyotakiwa kuwalinda raia na kuchangia uthabiti wa dunia na ndio sababu wanahitaji kufanya mazoezi pamoja.

Kiasi wanajeshi 2,800 kutoka nchi tisa wanachama wa Umoja wa Ulaya wakitumia  ndege 25 na manuwari sita walianza mazoezi ya wiki nzima kusini mwa Uhispania siku ya Jumatatu (Oktoba 16).

Soma zaidi: Umoja wa Mataifa waionya Israel juu ya kuizingira Hamas

Idara ya diplomasia ya Umoja wa Ulaya imesema luteka hizo zilizopewa jina LIVEX zinafanyika katika kambi ya jeshi la majini ya Rota karibu na mji wa kusini wa Cadiz.