1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Ukraine vyajipenyeza ndani ya Urusi

8 Agosti 2024

Urusi inakabiliana na vikosi vya Ukraine kwenye mapambano makali baada ya vikosi hivyo kufanikiwa kujipenyeza ndani ya mpaka wa kusini, ikiwa operesheni kubwa kabisa ya Ukraine ndani ya Urusi tangu vianze vita baina yao.

https://p.dw.com/p/4jDoy
Athari za mashambulizi ya Ukraine kwenye mkoa wa Kursk, Urusi.
Athari za mashambulizi ya Ukraine kwenye mkoa wa Kursk, Urusi.Picha: Acting Governor of Kursk Region Alexei Smirnov/Telegram/REUTERS

Kaimu Gavana wa mkoa wa Kursk, Alexey Smirnov, ametangaza hali ya hatari kwenye mkoa huo wa mpakani unaotambulika kuwa kituo kikuu cha usambazaji gesi asilia.

Wizara ya afya ya Urusi imesema raia 31, wakiwemo watoto sita, wamejeruhiwa, huku Gavana Smirnov akisema watu watano wameuawa kufikia sasa.

Hofu ya kutanuka kwa vita vya Urusi na Ukraine yaongezeka

Jeshi la Urusi linasema limeimarisha ulinzi kuzunguka kinu cha umeme wa nyuklia na mitambo yake minne kwenye mkoa huo wa Kursk.

Licha ya mafanikio hayo, Ukraine imepoteza eneo lenye ukubwa wa kilomita 420 za mraba tangu katikati ya mwezi Juni mwaka huu.