1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijana wajadili changamoto zinazolikabili bara la Afrika

25 Oktoba 2017

Mikutano kama ile ya jukwaa la kuibadilisha Afrika huwaleta pamoja baadhi ya vijana waafrika walio wabunifu kuzungumzia changamoto za siku za usoni zitakazolikumba bara hilo.

https://p.dw.com/p/2mVHB
Landwirtschaft Kenia Anbau von Mais
Akinamama barani Afrika wanaojishughulisha na kilimoPicha: Getty Images/AFP/Y. Chiba

Vicheko vilisikika wakati  marafiki wa zamani walipokuwa wakikutana kwa mara nyengine tena kwa matayarisho ya mkutano.

Waalikwa wamechanganyikana kuanzia Wakurugenzi watendaji hadi wawakilishi kutoka mashirika ya kikanda na kimataifa, lengo lao ni rahisi: kubadilishana mawazo ya namna ya kuiendeleza Afrika kuinukia katika muelekeo wa Kidunia kama bara lililo na nguvu. 

Awamu ya nne ya jukwaa hilo ilianzishwa kwa mjadala muhimu unaohusu changamoto katika mifumo ya kifedha ya Afrika katika matayarisho ya kukabiliana na uwezo wa kila eneo. Hii ikihusu ukuaji mkubwa wa kiuchumi kutokana na ongezeko la ghafla ya idadi ya watu wanaofanya kazi, ni namna siku za usoni ya Afrika inavyoonekana. Aidha ripoti ya matarajio ya idadi ya watu duniani ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mwaka huu inasema Afrika itakuwa na zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani ifikapo mwaka 2050. Hata hivyo katika mikutano ya kimataifa kama hii inaangalia suluhu na mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo.

UNFPA inaamini vijana ni muhimu katika kuleta mabadiliko

Logo UNFPA Bevölkerungsfond der Vereinten Nationen
Nembo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu

Natalia Kanem ni Mkurugenzi Mkuu wa  shirika la kukabiliana na idadi ya watu la Umoja wa Mataifa UNFPA, anavutiwa na namna Afrika inavyoelewa umuhimu wa kuwekeza kwa vijana. "Ukiwa na idadi ya watu iliyojaa vijana kama Afrika, ni muhimu kumuelimisha msichana mdogona kuhamimisha kuwa kijana mdogo ana uwezo wa ujasiriamali wa kujiangalia mwenyewe," alisema Natalia Kanem alipozungumza na DW. Ameongeza kuwa vijana wadogo wanaweza kwa urahisi kutayarishwa tena kupanga familia zao vizurina kuchangia maendeleo ya mataifa yao.

Aidha katika mataifa mengi ya kiafrika watu wanaishi katika mfumo wa kutegemea kile wanachopata ambacho huishia katika chakula tu. Suala juu ya usalama wa chakula kwa idadi ya watu inayokuwa linabakia muhimu katika ajenda ya serikali za Afrika zinazong'ang'ana kulisha watu wake waliyopo. Ni wazi kuwa kilimo cha chakula kitakuwa njia moja ya maisha katika  siku za usoni za watu wa Afrika.

Ibrahima Cheikh Diong, Muanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji washirika la ushauri na biashara lililo na makao yake makuu mjini Dakar nchini Senegal, ameliambia shirika la habari la DW kwamba kitu cha kwanza Afrika inayohitaji ni mabadiliko mapya, pamoja na kuelewa hadhithi yake na kuamua wapi inapotaka kuelekea na namna inavyoweza kufika inapotaka.

Janice da Grasa aliyehudhuria mkutano huo na anayetokea Cape Verde, amesema mikutano kama hii inampa nafasi ya kubadilishana mawazo na Waafrika wengine. "Tuko hapa kupata Afrika iliyo bora, na kwa sasa tunajadili juu ya ajenda za 2030. na nitakuwa hai na nataka kuona wakati huo Afrika tunayoipanga sasa, je tunaweza? tutaona." alisema Janice da Grasa.

Mwandishi: Amina Abubakar/DW

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman