1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijana 10,000 wakongamana Kigali Rwanda

10 Oktoba 2019

Jumla ya Vijana 10,000 kutoka nchi zote za Afrika na baadhi ya wawakilishi wa mashirika ya vijana ulimwenguni wamekutana Kigali kujadiliana mkakati wa kubadili mtazamo potofu kuhusu jinsi bara la Afrika linavyotazamwa.

https://p.dw.com/p/3R2TK
Ruanda Jugendliche Treffen in Kigali zu dreitägiger Konferenz
Picha: DW/Sylvanus Karemera

Hili ni kongamano la siku tatu ambapo viongozi wa serikali na wakuu wa serikali wanachanganua sababu za kulifanya bara la Afrika kuendelea kuonekana dhaifu mbele za macho ya walimwengu.

Karibu nchi zote zimetuma vijana wawakilishi kwenye kongamano hili. Mazungumzo yanayoendelea hapa ni kuhusu nafasi ya vijana katika kutatua changamoto zinazolikabili bara hilo. Moja ya changamoto zilizotangazwa na vijana hao ni ukosefu wa utawala bora barani Afrika kitu ambacho wanasema kimelifanya bara hilo kushindwa kupiga hatua ya haraka kwenye maendeleo ktk sekta mbalimbali.

Ni kongamano ambalo kwa siku yake ya kwanza usiku wa kuamkia leo liliongozwa na Rais Paul Kagame akiwa na viongozi wengine wakiwemo mawaziri wa vijana kutoka Afrika ambapo vijana walipata nafasi ya kuuliza maswali na kuonyesha changamoto zinazolikabili bara hilo.

Rais Kagame awashauri vijana kuugana kulipa bara la Afrika hadhi inayostahili

DR Kongo Beerdigung von Etienne Tshisekedi
Rais wa Rwanda Paul Kagame Picha: Presidence RDC

Rais Paul Kagame amewaambia vijana hao kwamba changamoto hizo zipo barani Afrika lakini itakuwa vigumu kuziondoa ikiwa hakutakuwepo na muungano wao.

"Hatua ya kuanzia inaweza kuwa nyumbani, yaani kama nyumbani kwako ni Mali, Cape Verde, Cameroun na kadharika yaanipaleulipotoka wakati unakuja hapa, baada ya hapo unakwenda kwa majirani na kwa kufanya hivyo maana yake unazidi kuungana na mwisho zile changamoto ambazo zilikuwa ni za nchi moja sasa zinakuwa za bara zimana hivyo kuzikabili inakuwa rahisi kwa sababu sasa sote tumekwishaungana na kuzikabili kwa pamoja,"alisema rais Paul Kagame.

Imetangazwa kwamba zaidi ya asilimia 60% ya wakazi wa Afrika ni vijana ambao kimsingi ndiyo wanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa ajira ambapo mwisho wa siku ndiyo wanarubuniwa na kujiingiza kwenye vitendo ambavyo ni hatari kwa usalama wa bara lao. Kongamano hili la siku tatu linajaribu kuzitazama changamoto na nafasi ya vijana katika kuzikabili.

Mwandishi: Sylvanus Karemera