1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Vifo nchini Sudan vyapindukia 2,000

16 Juni 2023

Vita vya Sudan hapo jana vimeingia mwezi wake wa tatu huku idadi ya vifo vikiripotiwa kupindukia elfu mbili. Haya ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na shirika moja la kunakili takwimu za mizozo.

https://p.dw.com/p/4Sft3
Umoja wa Mataifa umesema karibu watu 96 wameripotiwa kuuawa wiki hii huko El Geneina
Watu wakitembea katikati ya soko la El Geneina, Darfur Magharibi ambalo limeharibiwa vibaya, wakati mapigano yakiendelea nchini Sudan. Picha: Str/AFP

Idadi hii ya vifo imefikiwa baada ya gavana wa jimbo moja kuuwawa huko Darfur. Gavana huyo Khamis Abdullah Abakar aliuwawa saa chache baada ya kufanya mahojiano na kituo kimoja cha televisheni cha Saudi Arabia ambapo aliwakosoa wapiganaji wa RSF. Umoja wa mataifa umesema mashuhuda wamearifu kwamba gavana huyo aliuwawa na wanamgambo wa Kiarabu na wapiganaji hao wa RSF ambao wamekanusha kuhusika na tukio hilo na kulaani kuuwawa kwake. Wizara ya ulinzi ya Marekani imelaani machafuko hayo ya Darfur ikisema yanaleta kumbukumbu ya kilichotokea miaka 20 iliyopita katika mapigano yaliyosababisha vifo vya mamia kwa maelfu ya watu.