1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo kwa wajawazito ni changamoto Tanzania

17 Januari 2018

Wizara ya afya nchini Tanzania imesema vifo kwa wanawake wajazito bado ni changamoto kubwa. Mwaka 2005, vifo vya wajawazito vilikuwa ni 578 kwa vizazi hai laki moja na hadi kufikia mwaka 2015, vifo vilikuwa 556

https://p.dw.com/p/2r2OY
Kambodscha schwangere Frau im Krankenhaus
Picha: Imago/ZumaPress

Wizara ya afya nchini Tanzania imesema vifo kwa wanawake wajazito bado ni changamoto kubwa nchini humo ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa masuala ya afya imejizatiti kukabiliana navyo ili kuwa na uzazi salama katika taifa hilo linaloendelea.

Waziri wa afya nchini humo Ummy Mwalimu ameyasema hayo, alipozindua mpango mkakati wa miaka mitatu wa taasisi ya taaluma ya afya ya jamii, na kuongeza kuwa mwaka 2005, vifo vya wajawazito vilikuwa ni 578 kwa vizazi hai laki moja na hadi kufikia mwaka 2015, vifo vilikuwa 556 kati ya vizazi hai laki moja.

Hata hivyo waziri mwalimu ameiambia taasisi hiyo kuwa wakati serikali inapambana na kupunguza udumavu nchini humo, bado tatizo hilo lipo kwa kiasi kikubwa katika maeneo yenye kiwango kikubwa cha uzalishaji wa chakula ambayo ni Rukwa, Katavi pamoja na Njombe.

Katika magonjwa yasio ya kuambukiza imeonekana kuwa Watanzania wengi wameathirika hivyo serikali kuhitaji zaidi tafiti za kisayansi kwa kushirikiana na taasisi hiyo ili kukabiliana na magonjwa hayo, huku katika magonjwa ya kuambukiza malaria na kifua kikuu bado ni tatizo kwa taifa hilo.