1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo kutokana na maporomoko Ethiopia vyafikia 257

25 Julai 2024

Idadi ya vifo vilivyotokana na maporomoko ya ardhi nchini Ethiopia imeongezeka na kufikia watu 257.

https://p.dw.com/p/4iinW
Erdrutsch Äthiopien
Picha: Gofa Zone Government Communication Affairs Department

Kulingana na taarifa ya Umoja wa Mataifa hii leo, ambao umesema huenda idadi hiyo ikaongezeka hadi watu  500.

Janga hilo lilitokea siku ya Jumatatu baada ya mvua kubwa kunyesha kwenye kijiji kidogo cha Kencho Shacha Gozdi, kilichopo eneo la milimali katika katika jimbo la Ethiopia Kusini.

Shirika la masuala ya kiutu la Umoja wa Mataifa, OCHA limenukuu taarifa ya mamlaka za eneo la maafa, wakati mamia ya wakzi wakiendelea kutafuta manusura. Hii ni mara ya pili kutokea maafa mabaya kabisa nchini Ethiopia, taifa la pili kwa ukubwa barani Afrika.

OCHA imesema, zaidi ya watu 15,000 wanatakiwa kuhamishwa, ikiwa ni pamoja na watoto, wajawazito na wenye watoto watoto wachanga.