1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Washukiwa ugaidi wamekamatwa Austria

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQM

Polisi nchini Austria imesema,imewakamata watu 3 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda.Wizara ya mambo ya ndani ya Austria, mjini Vienna imesema,washukiwa hao wamekamatwa kuhusika na vitisho vilivyotolewa katika kanda ya video kwenye tovuti ya mtandao wa Internet. Katika kanda hiyo ya video,iliyotolewa mwezi wa Machi,Ujerumani na Austria zilionywa kuwa zitashambuliwa ikiwa tume za nchi hizo hazitoondoka Afghanistan.