1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vienna. Wanachama wa baraza la usalama wahitilafiana kuhusu Iran.

13 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDCu

Wanadiplomasia kutoka mataifa matano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa na wenye kura ya veto pamoja na Ujerumani wameshindwa kufikia makubaliano juu ya azimio la pamoja kuhusiana na mpango wa Iran wa kinuklia.

Wakati wa mazungumzo katika makao makuu ya shirika la umoja wa mataifa la udhibiti wa tekonlojia ya kinuklia IAEA mjini Vienna , China na Russia zinasemekana kuwa dhidi ya msimamo mkali wa Marekani katika suala hilo.

Nchi hizo mbili zinasema kuwa zinataka kungoja matokeo ya mazungumzo zaidi kati ya mkuu wa ujumbe wa majadiliano wa Iran Ali Larijani na mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana . Solana anajaribu kuishawishi Iran kukubali vivutio vya kiuchumi na kidiplomasia iwapo itasitisha urutubishaji wake wa madini ya Urani.