1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA : Utatuzi katika mzozo wa nuklea wa Korea Kaskazini

29 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnL

Shirika la masuala ya nuklea la Umoja wa Mataifa limeripoti kuridhika kwao baada ya kuuzuru mtambo wa kuzalisha plutonium wa Korea Kaskazini.

Taifa hilo la Kikomunisti limeahidi kuufunga mtambo huo hapo mwezi wa Februari chini ya makubaliano ya kupatiwa msaada ili nayo ikomeshe mpango wake wa silaha za nuklea.

Maafisa wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomu wamesema ingawa mtambo huo wa Yangbyon bado hakufungwa wameridhika na maendeleo yalifiokiwa kuelekea kwenye azma hiyo.

Mkuu wa timu hiyo ya Umoja wa Mataifa amesema kwamba upande wa Korea Kaskazini umekuwa na ushirikiano mkubwa sana.