1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA : Shirika la nuklea laalikwa Korea Kaskazini

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOl

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomu limesema kwamba limealikwa nchini Korea Kaskazini kwa mzungumzo juu ya mpango wa nuklea wa nchi hiyo.

Mkuu wa shirika hilo la IAEA Mohamed El Baradei amesema anataraji kujadili usitishaji wa mpango wa kutengeneza silaha za nuklea wa nchi hiyo na hatimae kukon’golewa kabisa kwa mitambo ya nuklea ya nchi hiyo.Hii ni ziara ya kwanza ya El Baradei nchini Korea Kaskazini tokea awe kiongozi wa shirika hilo la masuala ya nuklea la Umoja wa Mataifa hapo mwaka 1997.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon alikutana na El Baradei hapo awali amesema kwamba alikuwa na imani safari hiyo itatowa mchango mkubwa katika utekelezaji wa makubaliano yaliotiwa saini hivi karibuni.

Katika mazungumzo ya pande sita juu ya mzozo huo hapo mwezi uliopita Korea Kaskazini imekubali kuanza kuchukuwa hatua za kutokomeza silaha za nuklea.