1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vienna: Shirika la kimataifa la nguvu za atomiki-IAEA limeikosoa vikali Iran...

27 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFxY
kutokana na kuficha mipango ya kujipatia nguvu za atomiki.Hata hivyo shirika la IAEA halifikirii bado kuifikisha kadhia hiyo mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa.Shirika hilo la umoja wa mataifa limepitisha azimio ,baada ya maridhiano kufikiwa kati ya Marekani,Ujerumani,Ufaransa na Uengereza kufuatia majadiliano ya siku sita mjini Vienna.Licha ya lawama hizo lakini,shirika la IAEA limesifu pia utayarifu wa viongozi wa mjini Teheran wa kushirikiana na shirika hilo la kimataifa.Iran imesema iko tayari kutia saini itifaki ziada ya mkataba wa kutosambaza silaha za kinuklea-itifaki inayoruhusu kukaguliwa mitambo ya kinuklea ya nchi husika.Marekani haikufanikiwa katika madai yake kutaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya Iran.Serikali ya Marekani inaituhumu Iran kutumia mitambo ya nguvu za atomiki kwa lengo la kutengeneza silaha za kinuklea.Mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomiki IAEA Mohammed El Baradei amezisuta lakini hoja hizo.