1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA : Msichana alietekwa kwa miaka 8 apatikana

25 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDIJ

Msichana wa Austria alietekwa nyara wakati alipokuwa na umri wa miaka 10 na kushikiliwa mateka kwa miaka minane amepatikana wakati yule anayedhaniwa kuwa mtekaji wake amejiuwa na hiyo kutatuwa mojawapo ya kesi zilizokosa kufumbuliwa kwa muda mrefu kabisa nchini humo.

Polisi ya Austria imesema hapo jana kuwa msichana huyo alikuwa amepatikana akizubazubaa katika kitongoji kimoja cha Vienna siku moja kabla ya kutambuliwa na familia yake kuwa ni mtoto wao alietekwa nyara.

Msichana huyo amejitambulisha mwenyewe kuwa ni Natascha Kampusch na kutekwa kwake nyara hapo mwaka 1998 wakati akiwa njiani kwenda shule kulisababisha masikitiko makubwa na ni mojawapo ya upelelezi mkubwa kabisa wa polisi katika historia ya Austria.

Mtu anayedhaniwa kuwa mtekaji wake fundi wa simu Wolfgang Priklopil mwenye umri wa miaka 44 amejiuwa Jumaatano usiku kwa kujirusha chini ya treni mjini Vienna.

Shirika la habari la Austria APA limesema yumkini kukakuwepo na mtu wa pili katika utekaji nyara wa msichna huyo lakini imekataa kuzungumzia hilo.