1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vienna. Mataifa ya Ulaya yashindwa kuipeleka Iran katika baraza la usalama.

23 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEYa

Wanadiplomasia katika mkutano wa shirika la kimataifa la nishati ya Atomic mjini Vienna wameendelea kuwa katika mkwamo juu ya jinsi ya kulishughulikia suala la mpango wa kinuklia wa Iran, ambao mataifa ya magharibi yanahofia una lengo la kutengeneza silaha.

Marekani imekuwa ikilazimisha Iran ipelekwe katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa ajili ya uwezekano wa kuwekewa vikwazo. Lakini kutokana na upinzani kutoka Russia na China, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani zimeelezwa kuwa zimeacha madai kwamba shirika hilo la IAEA liipeleke Iran mara moja katika baraza hilo.