1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Marekani yaishutumu Iran

3 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFa8

Marekani imeishutumu Iran kwa kuwahadaa wakaguzi wa Umoja wa Mataifa juu ya silaha zake za nukclea. Wanadilpomasia wamesema shutuma hizo zimeishinikiza zaidi Tehran kukubaliana na masharti ya jumuiya ya Ulaya katika mazungumzo yatakayofanyika mwezi huu.

Hii leo rais Gorge Bush atafanya mazungumzo na waziri wake wa mambo ya nje Condolezza Rice juu ya iwapo Marekani ijiunge na jumuiya ya ulaya katika kuishawishi Iran kuachana na mpango wake wa silaha za nucklea.

Ufaransa,Uingereza na Ujerumani zilizoishutumu vikali Iran kwa kukosa kutekeleza ahadi ya kuachana na shughuli ambazo huenda zikatumika kuunda bomu la atomiki, wanaishawishi Iran kwa kutoa ahadi ya kuisadia kiuchumi na kisiasa lakini Iran imekataa ahadi hizo.

Hadi kufikia sasa Bush ameshikilia kwamba Iran iwekewe vikwazo na Umoja wa Mataifa.