1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vienna: Marekani yaishinikiza Ulaya kuhusu mpango wa Iran

20 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFzk

Washington na mataifa ya Ulaya, leo yametofautiana kwa umbali gani wakaguzi wa silaha za kinyulia wa Umoja wa Mataifa, wanastahili kushutumu kificho cha miaka 18 cha utafiti wa kinyuklia nchini Iran. Katika ripoti mpya kuhusu Iran, Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki Duniani, (IAEA), lilisema mnamo miongoni miwili liyopita, Tehran imekuwa ikivunja wajibu kadha wa mkataba wa Kutosambaza Silaha za Kinyuklia pamoja na kusafisha uranium. Wanachama wa bodi la IAEA wanakutana hii leo kujadili ripoti na muswada wa azimio lilizosambazwa na Ufaransa, Ujerumani na Uingereza, likiishutumu Iran kwa kushindwa kutekelezwa wajibu wake, kifungu ambacho kinaonekana hafifu machoni mwa Washington.