1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA : Korea Kaskazini ni tishilo la nuklea

19 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFVf

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki limeonya kwamba Korea Kaskazini inatowa tishio zaidi la nuklea kuliko hata Iran.

Mkuu wa shirika hilo Mohammed el Baradei amekiambia kituo cha televisheni cha CNN katika mahojiano kwamba Korea Kaskazini tayari ina plutonium ambayo inaweza kutumika kutengenezea bomu la nuklea wakati Iran imekuwa ikishukiwa tu kwamba ina mpango wa kutengeneza silaha za nuklea.Korea Kaskazini ilisitisha ushirikiano wake wote na shirika hilo la kusimamia masuala ya nuklea na kuwatimuwa wafanyakazi wake walioko nchini humo hapo mwezi wa Desemba mwaka 2002.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice ambaye yuko katika ziara ya siku sita barani Asia amewasili nchini Japani na anatazamiwa atataka kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya silaha za nuklea na Korea Kaskazini ambayo imeyakwamisha tokea mwezi wa Juni.