1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA Iran yabadili msimamo wake kuhusu mpango wake wa nuklia

16 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF35

Umoja wa Mataifa umesema kwamba Iran imebadili maelezo yake kuhusu mpango wake wa nuklia. Taifa hilo limekiri linajaribu kutengeneza silaha za nuklia. Katika ripoti yake, shirika la nishati ya nuklia ya umoja wa mataifa limesema serikali ya Tehran ilisema hapo awali kwamba ilikomesha shughuli za kutengeneza plutonium, kiungo muhimu cha bomu la nuklia mwaka wa 1993.

Wakati huo huo, wagombea wadhifa wa urais katika uchaguzi ujao nchini Iran wamekiri kwamba Iran haijasema ukweli kuhusu mpango wake wa nuklia. Rais wa zamani wa Iran, Akbar Hashemi Rafsanjani, aliyasema hayo katika mahojiano ya televisheni yaliyoonyeshwa na runinga ya BBC.

Alisisitiza kwamba nchi yake haitaufutilia mbali mpango wake wa nuklia. Wagombea wanane watashiriki katika kinyang´anyiro cha kuchukua nafasi ya rais wa sasa, Mohamed Khatami.