1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vienna. Iran kupelekwa katika baraza la usalama.

24 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEY7

Mataifa matatu ya umoja wa Ulaya yamewasilisha azimio katika shirika la umoja wa mataifa la nishati ya kinuklia ambalo linaweza kuipeleka Iran katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Azimio hilo linaiona Iran kuwa na hatia ya kukiuka mkataba wa kimataifa unazuwia kuenea kwa silaha za kinuklia .

Lakini azimio hilo litapelekwa tu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa baada ya mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la kimataifa la nishati ya Atomic , Mohammed El Baradei , atakapomaliza ripoti yake nyingine kuhusiana na mpango wa Iran wa Kinuklia.

Ujerumani, Uingereza na Ufaransa zinataka kuipeleka Iran mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusiana na shaka kuwa nchi hiyo inataka kutengeneza silaha za kinuklia.

Iran inasema kuwa mpango wake wa kinuklia ni kwa ajili ya matumizi ya amani . Magavana wa bodi ya shirika la IAEA watalijadili azimio hilo katika mkutano wao mjini Vienna baadaye leo.