1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Haider kuongoza chama kipya cha siasa kali za bawa la kulia

5 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFQG

Kiongozi wa siasa kali za bawa la kulia nchini Austria Jörg Haider amerejea katika siasa za taifa kuongoza chama kipya.Haider amesema atauongoza Muungano kwa Hatima ya Austria-chama kitakachochukua nafasi ya Chama cha Uhuru.Amesisitiza kuwa chama kipya kitabakia sehemu ya muungano unaotawala pamoja na Chama cha Watu cha kikonsavativ.Haider alizishtusha nchi za Ulaya,baada ya Chama cha Uhuru alicho kiongoza kushinda zaidi ya asili mia 25 ya kura katika uchaguzi wa mwaka 1999.Huo ulikuwa ushindi mkubwa kabisa kwa chama kinachofuata siasa kali za bawa la kulia,barani Ulaya tangu vita vikuu vya pili.