1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA. Austria yaidhinisha katiba ya Umoja wa Ulaya.

25 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFAF

Bunge nchini Austria limeidhinisha katiba ya Umoja wa Ulaya. Hatua hiyo inakamilisha kuidhinishwa kwa katiba hiyo baada ya serikali kufutilia mbali wito wa kufanyiwa kura ya maoni.

Austria haikuona umuhimu wowote wa kisiasa wa kura hiyo ya maoni, lakini Ufaransa na Uholanzi itafanya kura ya maoni juu ya katiba hiyo juma lijalo. Vyama vyote vya kisiasa nchini Austria vinaiunga mkono katiba hiyo ya jumuiya ya Ulaya.