1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoNigeria

Victor Boniface kuikosa michuano ya AFCON kutokana na jeraha

9 Januari 2024

Mshambuliaji wa Bayer Leverkusen raia wa Nigeria kuikosa michuano ya AFCON kutokana na jeraha.

https://p.dw.com/p/4b1To
Victor Boniface ataikosa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika
Victor Boniface ataikosa michuano ya Kombe la Mataifa ya AfrikaPicha: MB Media Solutions/IMAGO

Mfungaji bora wa klabu ya Bayer Leverkusen msimu huu inayoshiriki ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani - Bundesliga, Victor Boniface, ataikosa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, kutokana na jeraha.

Taarifa hiyo imetolewa na timu yake ya taifa ya Nigeria Super Eagles, japo hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.

Nafasi ya Victor Boniface sasa itachukuliwa na Terem Moffi.

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inaanza Jumamosi hii ya Januari 13 wakati Nigeria ambao ni mabingwa mara tatu wa michuano hiyo imepangwa katika kundi A pamoja na wenyeji Ivory Coast, Guinea-Bissau na Guinea ya Ikweta.

Mshambuliaji huyo wa Bayer Leverkusen ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram akiitakia kheri timu yake ya taifa.

Inaripotiwa kwamba Victor Boniface sasa atarudi mjini Leverkusen leo Jumanne japo klabu hiyo bado haijatoa tamko.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW