1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vatican yatuma mjumbe Moscow

27 Juni 2023

Mjumbe wa amani wa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, anatarajiwa kwenda Moscow kesho Jumatano akiwa na matumaini ya kutafuta suluhisho kwa hali ya sasa ya vita nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4T8Pl
Papst Franziskus
Picha: Stefano Spaziani/picture alliance

Hayo yameelezwa leo kupitia taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya Kanisa Katoliki mjini Vatican. 

Safari hiyo ya siku mbili ya Kadinali Matteo Zuppi mjini Moscow inafanyika wakati ikulu ya Kremlin inasawazisha hali ya mashaka iliyotokana na jaribio la uasi lililofanywa na kundi la mamluki la Wagner siku chache zilizopita.

Soma zaidi: Papa Francis akanusha kuwa anapanga kujiuzulu hivi karibuni

Taarifa ya Vatican imesema  Kadinali Zuppi ambaye tayari aliitembelea Ukraine mwezi uliopita, ataambatana na afisa mmoja wa sekretariati ya Vatican kwenye safari hiyo nchini Urusi. 

Lengo la ziara yake ni kuhimiza pande zote kujali ubinadamu na hataimaye kupata njia za kumaliza mzozo na kurejea kwa amani.