1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Kanisa Katoliki lalaani shambulio dhidi ya Trump

14 Julai 2024

Viongozi mbalimbali duniani wameendela kulaani jaribio la mauaji dhidi ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

https://p.dw.com/p/4iGod
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa FrancisPicha: Vatican Media/Independent Photo Agency Int./IMAGO

Trump alishambuliwa kwa risasi Jumamosi alipokuwa kwenye kampeni ya uchaguzi huko huko Pennsylvania.

Baada ya kauli za viongozi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, na mataifa mengine, uongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Vatican umelaani tukio hilo na kulielezea kama shambulio dhidi ya demokrasia.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema:

" Sote tulishuhudia hapo jana kwa mshtuko jaribio la mauaji ya kihalifu dhidi ya rais wa zamani na mgombea urais wa Marekani Donald Trump. Huu sio tu uhalifu mbaya, lakini pia ni jaribio la kuiua demokrasia ya Marekani."

Soma pia: FBI yachunguza jaribio la mauaji dhidi ya Trump

Trump mwenyewe amesema ni Mungu pekee ndiye aliyezuia jambo lisilofikirika huku akiwashukuru maafisa wa idara ya Ujasusi na maafisa wote wa usalama kwa hatua zao za haraka wakati wa shambulio hilo.