1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VALETTA: Wakimbizi wa Kiafrika wapotea baharini

31 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG2M

Wakimbizi 17 waliotaka kuingia Ulaya kwa njia isiyo halali hawajulikani waliko baada ya boti yao kuzama nje ya pwani ya Malta.Miongoni mwo,walikuwepo watoto 8 na mtoto mchanga mmoja. Nahodha wa uvuvi wa Kitaliana aliehusika katika juhudi ya uokozi,alipozungumza na redio ya Malta alisema,alipokuwa katika boti yake nje ya mwambao wa Malta,aliwaona wakimbizi hao wakiogelea baharini.Wanaume 8 na wanawake 5 waliokolewa na wamesema wanatokea Somalia.Siku moja kabla ya hapo,wakimbizi wengine 13 wa Ki-Afrika,kutoka kundi la watu 27,walifariki baharini walipojaribu kwenda Italia.Wakimbizi hao walitokea Libya.