1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uwindaji faru Afrika Kusini waongezeka 2023

27 Februari 2024

Serikali ya Afrika Kusini imesema imerekodi idadi ya faru 499 waliowindwa mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11 ikilinganishwa na mwaka 2022 licha ya juhudi za serikali kudhibiti biashara haramu ya pembe za ndovu

https://p.dw.com/p/4cxU1
Faru mwenye pembe na mtoto wake
Faru huwindwa kwa mapembe yakePicha: picture alliance/dpa/MAXPPP

Afrika Kusini inahifadhi takriban nusu ya faru weusi barani Afrika, ambayo pia ina idadi kubwa ya faru weupe walio katika hatari kubwa ya kutoweka.

Faru wamekuwa wakiwindwa kutokana na pembe zao, zinazotumika kwenye nchi za mashariki mwa bara la Asia kwa kutengeneza dawa za kienyeji na vito.

Soma pia: Ndovu barani Afrika waathirika na uwindaji haramu

Waziri wa Mazingira wa Afrika Kusini Barbara Creecy amesema mwaka 2023 faru 406 waliuwawa katika mbuga za wanyama za serikali na wengine 93 katika mbuga na mashamba binafsi.

Ameongeza kuwa simba 307 pia waliwindwa katika mbuga ya wanyama ya Hluhluwe-Imfolozi iliyopo katika mkoa wa mashariki wa KwaZulu-Natal.