1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uwanja wa ndege wa Hamburg wafungwa kwa sababu za kiusalama

5 Novemba 2023

Polisi nchini Ujerumani imewashauri wasafiri wasiutumie uwanja wa ndege wa Hamburg, kufuatia hali inayoendelea ya Baba mmoja kumshikilia mwanae mateka katika uwanja huo.

https://p.dw.com/p/4YQDS
Uwanja wa ndege wa Hamburg wafungwa kufuatia kisa cha utekaji
Uwanja wa ndege wa Hamburg wafungwa kufuatia kisa cha utekajiPicha: Daniel Bockwoldt/dpa/picture alliance

Uwanja wa Hamburg ulioko Kaskazini mwa Ujerumani umefungwa kwa wasafiri na hata safari za ndege kufutwa tangu Jumamosi usiku wakati mwanamume mmoja aliyejihami, alipouvamia uwanja huo kwa gari lake na kuvunja lango la kuingilia kabla ya kuanza kufyatua risasi hewani.

Polisi imesema mke wa mwanamume huyo awali aliripoti kuhusu utekaji nyara wa mtoto wao wa kike.

Mwanamume huyo aliye na miaka 35 anasemekana kumpokonya mkewe gari na kumchukua mtoto huyo wa miaka 4 na kuelekea moja kwa moja katika uwanja wa ndege alikosababisha tukio hilo.

Kwa sasa bado polisi na wanasaikolojia wanaendelea kuzungumza nae, lakini hakuna hata mtu mmoja aliyejeruhiwa katika mkasa huo.