1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UVUMI WA KINYAN'GANYIRO CHA MADARAKA KATIKA FDP

30 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CHOG

Gazeti la OSTTHÜRINGER ZEITUNG kutoka Gera laandika:

"Je, kuna kweli kinyan’ganyiro cha kuania uongozi ndani ya chama cha FDP? Hakuna kinyan’ganyiro hicho.Hakuna sio kwavile, mwenyekiti wa chama Bw.Guido Westerwelle, habishiki na kazi yake inawaridhisha wenzake chamani.Hakuna mtu anaeweza kweli kumpa changamoto barabara.Ndoto ya chama cha kileberali imeshatoweka

sawa nauwezo wake wa kufuata mkondo pekee wa kisiasa.Baada ya miaka 4 ya uongozi wa Bw.Westerwelle,wafuasi wa Free Democratic party wanajikuta pale walipokua hapo kabla.Yaani ni chama cha kukukipatia wingi wa viti vya kutawala kwa Muungano wa vyama vya CDU/CSU bila ya kuwa na umbo lake binafsi la kisiasa."huo ni uchambuzi wa OSTTHÜRINGER ZEITUNG.

Gazeti la kibiashara kutoka Düsseldorf:HANDELSBLATT laandika:

"Ladha ya kuonesha udume katika chama hiki cha kiliberali katika kumbomoa mwenyekiti wake imefikia kilele kipya.Ni tabia ilkiowaangusha wenyekiti wa hapo kabla-akina Klaus Kinkel na Wolfgang Gerhard.Sasa yabainika zamu ya Guido Westerwelle imewadia nae kubomolewa.

Mtu aweza kusema ikiwa chama hiki hakikua na usemi katika sera za mageuzi zilizojadiliwa hivi karibuni,sasa kimeangukiwa na bahati ya kuwa na mabishano yake binafsi ya kubomoana viongozi ili nacho kigonge vichwa vya habari hadharani. Mwenyekiti wa chama Westerwelle, haani mengi,kwani kwa sasa, hakuna kiongozi mwengine bora wa kumpiku chamani."

Ama gazeti linalochapishwa mjini Munich-ABENDZEITUNG linakichambua hivi kinyan’ganyiro hicho cha madaraka : Laandika kwamba, pale Westerwelle, alipochukua uongozi wa chama mikononi mwa Bw.Gerhardt,palikuwapo matumaini ndani ya FDP kwamba kila kitu kingepatikana.Wafuasi wa kawaida wa chama waliendelea kumfuata Bw.Gerhadt na kukipigia kura chama kama kabla.Na Bw.Westerwelle aliweza kujipatia wafuasi wapya.

Halafu ghafula mambo yakageuka kinyume chake:safari ya kubabaisha ya Bw.Westerwelle ikawastusha wafuasi wa zamani wa chama..............Chama cha FDP sasa kinabidi kuamua iwapo kiliomo ndani ya bahasa ndio muhimu zaidi au mapambo yake .

Gazeti la MORGENPOST kutoka Hamburg lajiuliza:

" Karne hii mpya ilioanza imetuletea nini mbali na muziki mbaya,George W.Bush na TV ya mtindo wa BIG BROTHER ?

Jibu ni siasa ya Ujerumani kufuata mtindo wa Bw.Westerwelle.Kwani, Bw.Westerwelle alikuja na mdundo mpya wa siasa za Ujerumani.

Tangu yeye kuanza kubobojoka mbele ya kila kikuza-sauti na kuwaudhi watu,tulianza kutanabahi,jinsi tunavyomkosa marehemu Franz Josef Strauss na sera zake kali,jazba na hamasa za Herbert Wehner na kujipa haki kila mara kwa Helmut Kohl."

Tumalizie kwa mada nyengine:Gazeti la LÜBECKER NACHRICHTEN linachangia hivi mjadala wa kuzidi kuzagaa kwa vumbi lisilionekana kwa macho katika miji ya Ujerumani.

Laandika :.................Tangu 1999 mwongozo uliotolewa na Umoja wa Ulaya kufuatwa ulikubaliwa na wote.Na tangu 2002 mwongozo huo umeiingizwa katika sheria za ujerumani na kuanza kazi mwanzoni mwa mwaka huo.Kwahivyo, kulikuwapo na muda wa kutosha kupunguza uvumi hilo linalosababisha vifo.Kwahivyo,hakuna aneamini sasa kutupiana lawama kwa serikali ya Shirikisho,zile za mikoa na wilaya,mashirika na viwanda vya magari .

Gazeti la KÖLNERSTADT-ANZEIGER latuhetimisha kwa kuandika kwamba, kila uchunguzi mpya unaofanywa unagundua kwamba ni barabara kulipiga vita vumbi linalotokana na misafara ya magari.Kinachoudhi mno ni kusitasita na kutochukua hatua kwa viwanda vya magari vya Ujerumani.......