1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yapanga kuidhinisha ombi la Finland kujiunga na NATO

16 Machi 2023

Maafisa wawili wa Uturuki wamesema kuna uwezekano mkubwa Bunge la nchi hiyo likaidhinisha mwezi ujao ombi la Finland la kujiunga na Jumuiya ya kujihami ya NATO.

https://p.dw.com/p/4Okkf
Türkei | Erdogan im türkischen Parlament
Picha: DHA

Taarifa hiyo imetolewa wakati Rais wa Finland Sauli Niinisto akitarajiwa hivi leo kufanya ziara nchini humo.

Sweden na Finland zilituma maombi mwaka jana kujiunga na NATO baada ya Urusi kuivamia Ukraine, lakini Sweden inakabiliwa na pingamizi kutoka Uturuki.

Finland yatumai kukubaliana na Uturuki kuhusu NATO

Ankara inasema Stockholm inawahifadhi wanachama wa vikundi vya kigaidi, jambo linalokanushwa na Sweden.

Mabunge ya nchi wanachama wote 30 wa NATO lazima yaidhinishe maombi ya uanachama kwa muungano huo. Mbali na Hungary, Uturuki ndiye mwanachama pekee ambaye bado hajaidhinisha maombi ya Finland na Sweden.