1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Uturuki yaahidi ujenzi mpya baada ya tetemeko la ardhi

15 Februari 2023

Uturuki imesema kuwa itabomoa majengo yaliyoharibiwa vibaya na tetemeko kubwa la ardhi lililoitikisa nchi hiyo na nchi jirani Syria wiki iliyopita na kuanza mara moja juhudi kubwa za ujenzi mpya.

https://p.dw.com/p/4NXAO
Erdbeben Türkei Kahramanmaras
Picha: ISSAM ABDALLAH/REUTERS

Serikali ya mjini Ankara imesema zaidi ya majengo 50,576 yameporomoka au kuharibiwa vibaya.

Idadi jumla ya vifo katika nchi hizo mbili imepanda hadi zaidi ya watu 41,000 na mamilioni wanahitaji msaada wa kiutu. Wengi wameachwa bila makaazi na kulazimika kukaa kwenye baridi kali.  

UN:Watoto milioni 7 wameathirika kote Uturuki na Syria

Wakati huo huo, Rais wa Syria Bashar al Assad amekaribisha kile alichokiita msimamo wowote chanya kutoka kwa mataifa ya Kiarabu, yakiwemo mengi yaliyovunja mahusiano na Damascus tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Matamshi yake yamejiri wakati wa mkutano na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Jordan Ayman Safadi mjini Damascus aliyeitembelea nchi hiyo kuonyesha mshikamano.