1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki na Urusi zimeingia katika kona

Saleh Mwanamilongo
4 Machi 2020

Viongozi wawili wa kibabe,Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na Vladimir Putin wa Urusi wameingia katika mchezo wa kisiasa,uliowaweka katika kona ambayo ni vigumu kujitoa, anasema Alexander Görlach.

https://p.dw.com/p/3YrGj
PK Erdogan und Putin
Picha: Reuters/Presidential Press Office/M. Cetinmuhurdar

Viongozi wawili wa kibabe, Rais Recep Tayyi Erdogan wa Uturuki na Rais Vladimir Putin wa Urusi wameingia katika mchezo wa kisiasa, uliowaweka katika kona ambayo ni vigumu kujitoa. Umoja wa Ulaya kwa upande wake, haujui cha kufanya kuhusiana na hali hiyo.

 Kile kinachoitwa  mkataba baina ya umoja wa Ulaya na Uturuki kuhusu wakimbizi kinasuasua. Maelfu ya wahamiaji wamerundikana kwenye mpaka wa Uturuki na Ugiriki baada ya rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan kuelezea wazi kwamba hawezi tena kuwazuwiya kuingia kinyume cha sheria kwenye nchi wanachama wa EU.

 Erdogan alithibitisha kwamba ''mamia ya maelfu yawahamiaji hao walikuwa njiani kwenda kwenye mapaka wa nchi yake na Ugiriki, na kutishia kwamba atawatuma zaidi ya milioni moja . lakini hadi sasa,kwa mujibu wa duru za kuaminika ni kwamba kuna wahamiaji 9000 hadi 30.000 waliokusanyika kwenye eneo la mpakani baina ya Uturuki na Ugiriki.

 

Hali ya hivi sasa inaonyesha wazi kinachotokea wakati wababe wanapokadiria vibaya yaliyo katika uwezo wao, na kujikuta katika mtego ambao ni vigumu kujinasua.  Erdogan anayejipambanua mwenyewe kama mbabe wa kikanda,alikuwa akitegemea  ungwaji mkono wa rais wa Urusi, Vladimir Putin, kwa sasa amendesha sera zake za nje kinyume na zile za Moscow ( Urusi).

 Waliokuwa washirika zamani ,leo wamekuwa maadui na makabiliano ya moja kwa moja yatazusha madhara yasiojulikana.

Portrait Prof. Dr. Dr. Alexander Görlach
Profesa Dr Alexander Görlach wa chuo kikuu cha Harvard.Picha: Harvard University/D. Elmes

Washirika wa Uturuki walionyesha ungwaji mkono wao kwa Erdogan na waliahidi ungwaji mkono mkono kwa nchi inayoungwa mkono na Urusi,ambayo imedondosha mabomu yanayouwa watu kwenye mahospitali,shule na maeneo ya kiraia nchini Syria,nakulazimisha watu wapatao milioni moja kukimbilia kaskazini mwa nchi hiyo.

 Kwa upande wake Uturuki inawapokea wakimbizi milioni 3.6 kutoka Syria.Lakini hali iko je ndani ya umoja wa Ulaya, ambako nchi wanachama ziliahidi kufanya kazi kwa pamoja huku zikitekeleza kanuni kwa manufaa ya jamii?

 Ukweli ni kwamba , toka mzozo wa wimbi la wakimbizi wa 2015, Umoja wa Ulaya haikufanikiwa kujiandaa kwa mzozo mpya nchini Syria.Na sasa umejikuta sawa na Uturuki zikitegemea hisani ya Urusi. Hakuna anayejua, huenda mzozo kati ya Urusi na Uturuki, ukamrudisha rais Erdogan kumaliza tofauti zake na Umoja wa Ulaya. 

 

Hatimae, watu wanataabika na siasa zilizopitwa na wakati za karne ya 19 zinazochezwa huko Syria. Pahali pa kueko na uingiliaji kati kwa ajili ya kumaliza mzozo wa kimataifa, urusi imedhani kwamba vita pekee ndivyo vitakavyomaliza mzozo wa Syria.

 Kuingineko, Putin ametumia nguvu alionayo kijeshi na tathmini kwamba ''kiongozi aliena nguvu'' ni yule anayetumia nguvu kwa kufumbua mizozo kuliko nchi za kiliberali ambazo zinatumia diploamisia ya kawaida.

 Erdogan ataelewa hatua kwa hatua maana ya kusitisha uhusiano na washirika wa zamani.

Lakini ulaya itazingatia kutosherehekea na kuchangia nguvu zake kwa Uturuki ilikupata suluhisho la tatizo lake la miaka mingi.