1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utawala wa Taliban wasema uko karibu kutambuliwa kimataifa

3 Februari 2022

Waziri wa mambo ya nje wa Afghanistan amesema utawala wa Taliban unakaribia kutambuliwa kimataifa, lakini muafaka wowote utakuwa chini ya masharti yao.

https://p.dw.com/p/46T1I
Afghanistan Wirtschaftskonferenz
Picha: Taliban Prime Minister Media Office/AP Photo/picture alliance

Waziri  Amri Khan Muttaqi ameelezea hayo katika mahojiano na shirika la habari la AFP, yakiwa ya kwanza tangu kurejea kutoka kwenye mazungumzo na mataifa ya Magharibi mjini Oslo, Norway.

Muttaqi pia ameihimiza Marekani kuachia mali za Afghanistan ili kusaidia kupunguza mzozo wa kiutu unaolikabilia taifa lake.

soma zaidi: Taliban wayasifu mazungumzo ya Oslo

Hakuna nchi iliyoitambua rasmi serikali iliowekwa baada ya Taliban kutwaa madaraka mwezi Agosti mwaka jana, lakini Muttaqi ameiambia AFP jana jioni, kwamba watawala wapya wa Afghanistan wanaanza kukubalika taratibu.

Amesema mataifa kadhaa yalikuwa yanaendesha balozi zao mjini Kabul, na nyingine zaidi zinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni. Mazungumzo ya Norway ndiyo yalikuwa ya kwanza kufanyika nchi ya magharibi yakiwahusisha Taliban.