1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Somaliland yasema haina mpango wa kujiunga tena na Somalia

25 Septemba 2023

Utawala wa Jimbo lililojitenga la Somaliland umesema hauna mpango wowote wa kujadili kujiunga tena na Somalia, ukikanusha kauli ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni aliyesema atakuwa mpatanishi kati ya pande hiyo mbili

https://p.dw.com/p/4WlXN
Bendera ya taifa ya Somaliland
Bendera ya taifa ya SomalilandPicha: Valerio Rosati/PantherMedia/IMAGO

Serikali ya Somaliland imesema katika taarifa yake hapo jana kuwa, mazungumzo yoyote yatayofanyika kati ya Somaliland na Somalia hayatojadili masuala ya muungano, bali namna nchi hizo mbili zinavyoweza kusonga mbele.

Somaliland bado haijatambuliwa kimataifa

Somaliland ambayo kwa miongo mitatu imekuwa na amani huku nchi jirani ikikabiliwa na vita, ilitangaza uhuru wake kutoka kwa Somalia mnamo mwaka 1991, lakini haijapata kutambuliwa kimataifa.