1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utawala wa kijeshi wa Niger waituhumu Ufaransa kula njama

31 Julai 2023

Utawala mpya wa kijeshi nchini Niger umeituhumu Ufaransa, ambayo ni mkoloni wa zamani wa taifa hilo, kuwa inapanga "kutumia nguvu za kijeshi" ili kuurejesha madarakani utawala uliopinduliwa wa Rais Mohammed Bazoum.

https://p.dw.com/p/4UanN
Screenshot DW Sendung Niger
Picha: DW

Tuhuma hizo zilitolewa katika taarifa iliyosomwa kupitia televisheni ya taifa na Kanali Amadou Abramane, mmoja wa wanajeshi waliopanga mapinduzi ya wiki iliyopita. 

Taarifa hiyo ilisema  Ufaransa kwa kushirikiana na baadhi ya raia wa Niger wamefanya kikao cha kutafuta idhini ya kufanya mashambulizi dhidi ya utawala mpya mjini Niamey. 

Soma: Niger yaituhumu Ufaransa kula njama za kuurudisha utawala wa rais aliyepinduliwa

Ufaransa haijasema chochote kuhusu tuhuma hizo, lakini Rais Emmanuel Macron aliarifu siku ya Jumapili (Julai 31) kwamba nchi yake ingelichukuwa hatua iwapo raia au maslahi yake yangelihujumuiwa nchini Niger. 

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) iliuonya utawala mpya nchini Niger kuwa ungelikabiliwa na vikwazo vikali vya kiuchumi na uwezekano wa kutumia nguvu iwapo usingelirejesha mamlaka ya taifa hiyo chini ya misingi ya katiba.