1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utanuzi wa Umoja wa Ulaya kuleta Siasa Mpya ya Maendeleo

28 Mei 2004

Utanuzi wa Umoja wa Ulaya mwanzoni mwa mwezi huu umebadili pia siasa ya maendeleo ya nchi jumuiya hii. Kwa pamoj, Umoja wa Ulaya na wanachama wake kila mwaka hulipa EURO Biliyoni 26 kugharimia misaada ya maendeleo duniani.

https://p.dw.com/p/CEI2

Kiwango hicho ni nusu ya misaada yote ya maendeleo inayotolewa kote duniani kila mwaka. Na kwa kujiunga wanachama wapya kumi hivi sasa. kiwango hicho kitazidi kuongezeka. Lakini swali ni, je utakuwaje uhusiano huu mpya kati ya nchi 25 zanachama wa Umoja wa Ulaya na jumla ya nchi 143 zinazoendelea? Ahmed Mohamed anaendelea kusimulia:

Kwa hakika hiyo haikuwa mada ya mbele katika mijadala ya kuwania uanachama mpya katika Umoja wa Ulaya (UU), japokuwa ni mada iliyozidi kujitokeza mnamo miezi ya michache ya nyuma,hasa hasa katika mjadala wa hadharani ulioandaliwa na mashirika manne mjini Bonn. Wawakilishi hao kutoka sekta za siasa na utafiti waliwafikiana kuwa utanuzi wa UU utaleta vipimo vipya katika siasa ya maendeleo. Kwa mujibu wa Bibi Heike Pörksen, mshauri wa kitaalamu katika Wizara ya Maendeleo ya Ujerumani:

Litabidi liulizwe swali ikiwa nchi hizo zinazoendelea ziongezewe misaada ya maendeleo kuanzia mwaka 2007 wakati itakapokusanywa bajeti mpya ya matumizi ya maendeleo. Anasema khofu iliyopo ni kuwa kwa sababu baadhi ya wanachama wapya watabidi pia kutegemea misaada ya nchi tajiri za UU, uko uwezekano kuwa nchi zinazoendelea zitapunguziwa misaada ya maendeleo. Ndiyo maana anasema wao wanasititiza kuwa misaada hiyo ya maendeleo isipunguzwe ili kiweko kipimo kile kile cha kupigana na umasikini. Lakini kutokana na maarifa yao wenyewe ya kihistoria wanachama wapya wameweka mbele mambo mengine muhimu, kwa mfano siasa ya usalama, siasa ya kiuchumi pamoja na juhudi za kidemokrasi katika nchi zinazoendelea. Kwa mfano Marian Caucik, mkuu wa Jumuiya ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Slovakia anasema kuwa:

Nchi mpya zanachama zitashirikiana zaidi na nchi ambazo zilikuwa na ushirikiano nao tangu zamani. Kwa maneno mengine ushirikiano wao utaendelezwa na nchi za Balkan na nchi za Umoja wa zamani wa Kisoviyeti, na pia nchi za Kiafrika au nchi za Asia. Kwa maoni ya Bibi Heike Pörksen kutoka Wizara ya Maendeleo ya Ujerumani ziko nchi nyingi mpya zamnachama wa UU zinazounga mkono kuongezewa nchi za Kiafrika na Asia misaada ya maendeleo na hafikiri kuwa UU utabadili siasa yake katika sekta hiyo na kuzipunguzia nchi hizo misaada. Zilipojiunga na UU nchi mpya zanachama zimeahidi kuwa washirika wenye haki sawa katika Mpango wa Misaada ya Maendeleo ya Umoja huo, japokuwa kwa sasa ni bado midogo mno michango yao katika fuko la misaada ya maendeleo. Lakini michango hiyo imekusudiwa kuongezwa hapo siku za usoni, mwongezeka ambao ni mzigo mzito wa kifedha kwa nchi hizo ikiwa ni pia vigumu kuwapata raiya wa nchi mpya zanachama kuridhia mwongezeko mpya kama huo, kwa sababu bado hakuna harakati nyingi za kutangaza umuhimu wa ushirikiano kama huo wa maendeleo anasema Oboaya Baaranye kutoka Shirika la Maendeleo la Hungary, akisisitiza pia nchi hizo pia zina matatizo yao wenyewe wa kijalii. Msaada wanaoweza kutoa ni kuchangia katika usambazaji wa elimu ya kikazi.Lakini mojawapo ya sekta ambamo nchi mpya zanachama zina maarifa makubwa ni katika sekta ya kupambana na kusuluhisha misukosuko ya zamani, zikiweza kuzisaidia nchi zinazoendelea kupambana na kuondoa matatizo yao ya zamani. Ibolya Baranyi anasema shiria lake mara kwa mara hupokea maswali ya misaada ya ushauri kutoka kwa nchi zilizotawaliwa zamani na wakoloni. Hata hivyo kwa sasa ni bado mapema kubashiriki kitu juu ya nafasi za kufanikiwa muundo huo mpya wa ushirikiano kati ya nchi mpya zanachama za UU na nchi zinazoendelea.