1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utafiti: Viwango vya demokrasia vimeshuka ulimwenguni

Sylvia Mwehozi
15 Februari 2024

Kitengo cha utafiti cha shirika la Economist, kimesema kuwa viwango vya demokrasia kote ulimwenguni, vilishuka mwaka uliopita, katikati mwa vita na ukandamizaji wa kimabavu.

https://p.dw.com/p/4cPfL
Guatemala
Bango linalosomeka bila uandishi wa habari hakuna demokrasia huko GuatemalaPicha: Johan Ordonez/AFP/Getty Images

Kitengo cha utafiti cha shirika la Economist, kimesema kuwa viwango vya demokrasia kote ulimwenguni, vilishuka mwaka uliopita, katikati mwa vita, ukandamizaji wa kimabavu na kupungua kwa uaminifu katika vyama vikuu vya kisiasa.

Utafiti huo unasema ulimwengu umeingia katika enzi ya migogoro na mikondo ya vita kuu ya siku zijazo tayari inaonekana. Aidha utafiti huo uliotolewa leo, umebainisha kwamba vita vya sasa vimejikita zaidi katika nchi ambazo demokrasia haipo au zipo katika matatizo.

Kitengo hicho cha utafiti kimedokeza pia kuwa kumekuwa na ongezeko la hatua kali za kupinga wahamiaji katika nchi nyingi na kuongeza kwamba hali ya kisiasa barani Amerika na Ulaya imezidi kuwa na mgawanyiko.

Norway, New Zealand na Iceland ziko nafasi ya juu katika demokrasia wakati Korea Kaskazini, Myanmar na Afghanistan zikishika mkia.