1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usitishaji mapigano waanza rasmi Ukraine

15 Februari 2015

Usitishaji mapigano umetangazwa rasmi mashariki mwa Ukraine saa sita usiku wa kuamkia Jumapili (15.02.2015) na kufufua matumaini ya utulivu katika mzozo ambao umesababisha zaidi ya watu 5,000 kupoteza maisha.

https://p.dw.com/p/1Ebyb
Ukraine Kämpfe Armee Donezk
Silaha zimesita kushambulia Ukraine masharikiPicha: Volodymyr Shuvayev/AFP/Getty Images

Lakini katika muda wa masaa mawili baada ya usitishaji mapigano kuanza, pande zinazopigana tayari zilikuwa zinatupiana upya lawama.

Katika siku zijazo mtazamo wa kimataifa utalenga eneo muhimu la usafiri wa treni katika mji wa Debaltseve, ambako majeshi ya serikali ya Ukraine kwa wiki kadhaa yamekuwa yakipambana kuulinda mji huo dhidi ya mashambulio makali ya wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi na wanaotaka kujitenga.

Ukraine Soldaten Raketenwerfer Raketen auf Donezk
mapambano kabla ya kusitisha mapiganoPicha: Reuters/Alexei Chernyshev

Wizara ya mambo ya kigeni nchini Marekani imesema picha zinazopatikana kutoka mashariki mwa Ukraine zinatoa "ushahidi wa kutosha" kwamba jeshi la Urusi limeweka idadi kubwa ya silaha pamoja na vifaa kadhaa vya kurushia makombora kuzunguka mji wa Debaltseve kupambana na majeshi ya Ukraine.

"Tuna imani kwamba haya ni majeshi ya Urusi, na sio ya wapiganaji wanaotaka kujitenga," msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni Jen Psaki ameeleza katika taarifa Jumamosi (14.02.2015).

Rais atoa amri ya kusitisha mapigano

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko ametoa amri ya kusitisha mapigano katika hotuba aliyoitoa kupitia televisheni akivitaka vikosi vya jeshi la nchi hiyo kusitisha mapigano dakika moja baada ya muda uliowekwa wa kusitisha mapigano kumalizika usiku wa manane kuamkia leo Jumapili.

Ukraine Konferenz in Minsk Poroschenko
Rais Petro Poroshenko wa UkrainePicha: AFP/Getty Images/K. Kudryavtsev

Shutuma za ukiukaji wa makubaliano zilifuata mara baada ya hapo.

Mkuu wa idara ya usalama wa taifa nchini Ukraine, Valentyn Nalyvaichenko, amesema ukiukaji mara moja umeripotiwa kiasi ya dakika 50 baada ya muda wa mwisho wa kusitisha mapigano kufika.

Makombora kadhaa yalifyatuliwa kutoka katika eneo ambalo Nalyvaichenko ambalo liko chini ya udhibiti wa kikosi cha Cossack kinachodhibitiwa na raia wa Urusi.

Wakati huo huo, waasi wameishutumu Ukraine kwa kutumia silaha muda mfupi baada ya usiku wa manane.

Lawama kila upande

Shirika la habari la Donetsk, chombo kinachotumiwa na wanaotaka kujitenga, limemnukuu afisa wa kijeshi mwandamizi wa waasi Eduard Basurin akisema majeshi ya Ukraine yaliyoko katika mji wa Debaltseve yameshambulia kwa makombora na mizinga maeneo ya waasi.

Deutschland Münchner Sicherheitskonferenz 2015 MSC Sergei Lawrow
Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei LavrovPicha: Müller / MSC

"Kwa manufaa ya uzuwiaji wa vifo vya raia, silaha zinazolenga zinawekwa kuelekea maeneo ya adui," Basurin amenukuliwa akisema.

Saa chache kabla ya muda wa kusitisha mapigano kufika zilishuhudia mapigano makali kuzunguka mji wa Debaltseve, wakati majeshi ya Ukraine yalifanya juhudi za haraka kupata udhibiti katika barabara kuu inayounganisha mji huo na vikosi vinavyosaidia nje ya mji huo.

Akizungumza na mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov kwa simu jana Jumamosi, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry ameeleza wasi wasi wake juu ya kile alichokiita juhudi za Urusi na wapiganaji wanaotaka kujitenga kuutenga mji wa Debaltseve kabla ya muda wa kusitisha mapigano kufika.

USA Dalai Lama beim National Prayer Breakfast 5.2.2014
Rais Barack Obama wa MarekaniPicha: picture-alliance/AP/Evan Vucci

Wapiganaji wanaotaka kujitenga wanasisitiza kwamba wameuzingira kabisa mji wa Debaltseve, ambao wanasema ni hali inayowaruhusu kudai eneo hilo ni lao.

Lakini rais Poroshenko amesema katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja katika televisheni kwamba barabara kuu kuelekea katika mji huo bado iko wazi na kwamba vikosi vya jeshi la Ukraine vimepelekewa mahitaji ya silaha na risasi.

Rais wa Marekani Barack Obama amempigia simu mwenzake wa Ukraine Petro Poroshenko jana Jumamosi kuelezea "wasi wasi wake mkubwa " na "mshikamano" kuhusiana na machafuko yanayoendelea wakati usitishaji mapigano ukianza mashariki mwa Ukraine.

Mwandishi: Sekione Kitojo/afpe/ape

Mhariri: Elizabeth Shoo