1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yazuia mashambulizi usiku kucha katika Bahari Nyeusi

25 Julai 2023

Urusi imesema leo kuwa imezuia mashambulizi ya usiku kucha ya ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya meli yake ya kijeshi iliyokuwa ikishika doria katika Bahari Nyeusi ambapo hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka.

https://p.dw.com/p/4ULSc
Ukraine | Getreideabkommen | Frachtschiff Tq Samsun Odessa - Istanbul
Picha: Yoruk Isik/REUTERS

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kuwa jeshi la Ukraine limefanya mashambulizi hayo kwa kutumia ndege mbili zisizokuwa na rubani dhidi ya meli ya doria ya Sergei Kotov.

Wizara hiyo imeongeza kuwa Urusi ilitumia silaha za kawaidakwenye meli hiyo kuharibu ndege hizo kutoka umbali wa takribani kilomita moja. Hata hivyo, hakuna aliyejuruhiwa na meli hiyo inaendeleza doria yake.

Soma pia:Urusi kuchukua jukumu la kusafirisha nafaka barani Afrika

Meli hiyo inasemekana ilikuwa inashika doria yake umbali wa kilomita 370, kusini magharibi mwa Sevastopol, bandari muhimu ya Urusikatika Rasi ya Crimea iliyotekwa na Urusi mnamo mwaka 2014.