1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Maelfu ya watu wakimbia Kharkiv kutokana na mashambulizi

13 Mei 2024

Urusi imechukua udhibiti wa vijiji vinne zaidi katika mkoa wa Kharkiv huku maelfu ya wakaazi wakihamishwa kutoka mkoa huo ulioko kaskazini mashariki mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4flgW
Moshi ukifukuta baada ya shambulio la kombora la Urusi mkoa wa Kharkiv, kaskazini mashariki mwa Ukraine.
Moshi ukifukuta baada ya shambulio la kombora la Urusi mkoa wa Kharkiv, kaskazini mashariki mwa Ukraine.Picha: Vyacheslav Madiyevskyy/Ukrinform/picture alliance/abaca

Gavana wa Kharkiv Oleg Syniehubov amesema zaidi ya watu 4,000 wamehamishwa na kwamba "maeneo yote" yaliyo mpakani na Urusi yanashambuliwa.

Mamlaka imeripoti vifo vya raia kadhaa katika mashambulizi hayo, kifo cha hivi karibuni kikiwa cha mzee wa miaka 63 aliyeuawa kazika kijiji cha Glyboke.

Soma pia: Watu 17 wajeruhiwa katika shambulizi la Ukraine nchini Urusi

Mkuu wa jeshi la Ukraine Oleksandr Syrskii amekiri kuwa vikosi vyake vinakabaliwa na "wakati mgumu" japo wanaendelea kukabiliana na wanajeshi wa Urusi.

Tangu mwezi Machi, Urusi imezidisha mashambulizi nchini Ukraine na kulenga miundombinu ya nishati na makaazi ya watu.