1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yawafukuza mabalozi wawili wa Marekani

14 Septemba 2023

Urusi imesema leo kwamba imewafukuza wanadiplomasia wawili wa Marekani kwa tuhuma za kushirikiana na mfanyakazi wa zamani wa ubalozi mdogo wa Marekani Robert Shonov ambaye Moscow inamtuhumu kwa ujasusi.

https://p.dw.com/p/4WLZU
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin Picha: Alexander Kazakov/Russian President Press Office/dpa/picture alliance

Shonov aliyekuwa akifanya kazi kwenye ubalozi huo mjni Vladivostok alidaiwa kuwapa taarifa wanadiplomasia wa Marekani, zinazohusiana na mzozo kati ya Urusi na Ukraine, ingawa Washington inakana tuhuma hizo.

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema wanadiplomasia hao wawili Jeff Sillin na David Bernstein walifanya shughuli haramu kwa kushirikiana na Shonov ambaye ni raia wa Urusi.

Soma pia:Rais wa Urusi, Vladimir Putin na kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong Un wafanya mazungumzo

Tayari Moscow imemuarifu balozi wa Marekani nchini humo, na wanadiplomasia hao wamepewa siku saba za kuondoka chini ya hadhi ya watu wasiotakiwa kuingia tena Urusi.