1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Urusi yaushambulia mji wa Lviv magharibi mwa Ukraine

Sylvia Mwehozi
5 Septemba 2024

Urusi imeushambulia mji wa Lviv magharibi mwa Ukraine siku ya Jumatano, na kuwaua watu saba wakiwemo watoto na kuharibu majengo ya kihistoria. Watu wanne wa familia moja wamefariki.

https://p.dw.com/p/4kHw6
Ukraine | Lviv
Wafanyakazi wa dharura katika mji wa Lviv magharibi mwa Ukraine wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyeuawa katika shambuliziPicha: Roman Baluk/REUTERS

Urusi imeushambulia mji wa Lvivmagharibi mwa Ukraine siku ya Jumatano, na kuwaua watu saba wakiwemo watoto na kuharibu majengo ya kihistoria. Miongoni mwa waliokufa ni watu wanne kutoka familia moja, mwanamke na binti zake watatu, na kumwacha baba yao akiwa manusura pekee. Meya wa jiji hilo amesema shambulio hilo la kombora pia limejeruhi watu 64 na kuharibu shule na vituo vya matibabu pamoja na majengo katika kituo cha kihistoria cha Lviv.

Shambulio hilo limefanyika wakati mawaziri kadhaa wa Ukraine, akiwemo mwanadiplomasia mkuu Dmytro Kuleba, wakijiuzulu. Rais Volodmyr Zelensky wa Ukraine amesema hatua hiyo ni sehemu ya mabadiliko ambayo yataleta nguvu mpya katika serikali. Urusi imezidisha mashambulizi yake ya anga dhidi ya Ukraine tangu Kyiv ilipoanzisha mashambulizi ya kuvuka mpaka katika eneo la Kursk nchini Urusi mwezi uliopita.