1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge Ukraine laridhia kujiuzulu Naibu Waziri Mkuu

4 Septemba 2024

Bunge la Ukraine limeridhia hatua ya kujiuzulu naibu waziri mkuu, waziri wa mikakati ya viwanda pamoja na mawaziri wengine wawili.

https://p.dw.com/p/4kHO7
Jengo la Bunge la Ukraine
Jengo la Bunge la UkrainePicha: SERGEI SUPINSKY/AFP

Kikao cha bunge kilichofanyika leo kilimalizika bila ya suala la kujiuzulu kwa waziri wa mambo ya nje Dymytro Kuleba kujadiliwa.

Rais Volodymyr Zelensky amesema serikali yake inahitaji nguvu mpya na hatua yake ya kufanya mageuzi ya baraza la mawaziri inahusiana na mpango wa kuimarisha hali ilivyo kwenye maeneo mbalimbali.

Soma pia:Naibu waziri wa ulinzi wa Urusi akamatwa kwa madai ya rushwa

Mpango wa Rais Zelensky wa kutaka kufanya mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri, umewafanya mawaziri chungunzima kujiuzulu.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW